Habari

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Imetumwa: Aug 31 , 2016


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


OFISI YA WAZIRI MKUU


KAZI, VIJANA, AJIRA NA WATU WENYE ULEMAVU


Maadhimisho ya Miaka Kumi na Tano (15) ya Kuanzishwa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA)


Dodoma, 30 Augusti 2016


Taarifa kwa Vyombo vya Habari


Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) ulianzishwa kama sehemu ya programu ya Marekebisho ya Huduma za Umma (PSRP) chini ya Sheria ya Wakala za Selikali Na. 30 ya 1997. OSHA ilizinduliwa rasmi tarehe 31 Agosti 2001 kwa lengo la kuboresha Afya na Usalama (Ustawi) wa wafanyakazi mahali pa Kazi. Lengo hilo litafikiwa kwa kuhamasisha Waajiri na Wafanyakazi kuzingatia misingi ya uboreshaji Afya na Usalama Mahali pa Kazi ili kupunguza ajali na magonjwa yatokanayo na kazi na hatimae kuongeza tija. Leo hii ni miaka 15 tangu kuanzishwa kwa Wakala wa Usalama na Afya mahali pa Kazi (OSHA).

Dhima ya Wakala ni kuhamasisha na kuhimiza taratibu za kazi zinazozingatia Usalama na Afya mahali pa Kazi ili kuzuia ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kwa lengo la kuongeza tija katika sehemu ya kazi. Dira ya Wakala ni kuwa Wakala wa Serikali wenye uwezo wa kutoa huduma bora katika kushauri, kusimamia na kuhakikisha viwango vya Usalama na Afya mahali pa Kazi vinazingatiwa.

Tangu kuanzishwa kwa Wakala, Wakala umekuwa ukitoa huduma mbalimba za Afya na Usalama kazini. Baadhi ya huduma hizo ni kama zifuatazo:

1.      Kusajili  sehemu za kazi

2.      Kutoa leseni za kukidhi matakwa ya Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi.

3.      Kufanya kaguzi za Usalama na Afya mahali pa Kazi, ikiwemo Ukaguzi wa Ujumla (General Inspections), Ukaguzi wa mitambo, Ukaguzi wa Umeme, Ukaguzi wa mazingira mfano vumbi,kelele n.k.

4.      Kutathmini hatari za Kiusalama na Kiafya sehemu za Kazi,

5.      Kuhakiki/kuidhinisha ramani na michoro ya sehemu za kazi,

6.      Kupima afya ya uwezo wa kufanyaka kazi kwa wafanyakazi

7.      Kufanya utafiti na kutoa mafunzo ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

8.      Uchunguzi na uidhinishaji wa michoro na ramani mbalimbali za majengo ya maeneo ya kazi;

9.      Kufanya Uchunguzi wa Ajali na magonjwa yatokananyo na Kazi

Mafanikio

Tangu kuanzishwa kwa Wakala miaka 15 iliyopita kumekuwepo kwa mafanikio mbalimbali. Yafuatayo ni baadhi tu ya mafanikio hayo;

1.      Kuongezeka kwa idadi ya watimishi kutoka jumla ya watumishi 46 katika mwaka wa fedha 2006/7 hadi kufikia watumishi 113 katika mwaka wa fedha 2015/16.

2.      Kuongezeka kwa idadi ya sehemu za kazi zilizosajiliwa. Hadi kufikia sasa wakala umesajili sehemu za kazi zipatazo 12,519 likiwa ongezeko la idadi mpya za kazi zipatazo takribani 2,000 kwa mwaka uliopita.

3.      Kuongezeka kwa idadi ya wafanyakazi waliochunguzwa afya zao kutoka 15,418 katika mwaka wa fedha 2007/8 hadi kufikia 66,889 katika mwaka wa fedha wa 2015/16.

4.      Kuanzishwa kwa kozi ya Taifa ya Afya na usalama mahali pa kazi kwa maafisa wa usalama na afya mahali pa kazi ambapo mpaka sasa idadi ya wahitimu hao imefikia zaidi ya 1,800.

5.      Wakala umeratibu uridhiaji wa mikata ya Afya na usalama mahali pa kazi ya ILO ipaya sita (6) na kutunga kanuni nne (4) za afya na sula hadi kufikia mwisho wa mwaka wa fedha wa 2015/16.Aidha katika kipindi kifupi cha mwaka huu wa fedha tayari kanuni mbili zimesainiwa., kufanya kanuni ziwe 6.

6.      Wakala umeboresha maslahi kwa watumishi wake kwa kuweka vivutio vya masilahi (incetive scheme), kutoa chai na chakula cha mchana, kuanzisha mazoezi ya kujenga miili kwa watumishi

7.      Wakala umezindua mkataba wa huduma bora kwa mteja tangu mwaka wa fedha 2013/14 , na kutoa mafunzo ya huduma bora kwa mteja kwa watumishi wote.

8.      Wakala umefanikiwa kuongeza vitendea kazi na nyenzo nyingine ambazo zimewawezesha kusogeza huduma kwa wanainchi kwa kufunga ofisi mikoani kufikia uwepo wa ofisi za OSHA katika mikoa 10 hadi sasa, na ofisi tatu nyingine ziko mbiyoni

9.      Wakala umeweza kuongeza kampeni za utoaji elimu na kuongeza uelewa wa umuhimu wa usalama na afya mahali pa kazi, na hivyo kuhamasisha wafanyakazi na jamii kulinda, na kutetea afya na usalama wao wawapo kazini.

10.   Wakala umeweza kuziba pengo la ufinyu wa watumishi wa kushirikiana na sekta binafsi  (private inspectors ) na kuongeza uwigo wa kaguzi na hivyo kusogeza huduma kwa watanzania wengi zaidi .


Changamoto

Pamoja na mafanikio, changamoto mbalimbali zimekuwa zikijitokeza katika kutekeleza majukumu ya wakala kama vile idadi isiyotosha ya watumishi ukilinganisha na mahitaji ya nchi.  Ufunyu wa majengo ya Ofisi,. Kudorola kwa hali ya usalama katika sekta ya wajasiriamali kwani hawamudu kulipia gharama za ukaguzi na mafunzo ya Usalama na Afya. Halikadhalika bado Uelewa wa masuala ya Afya na Usalama baina ya wadau haujaridhisha.

Matarajio ya Baadae

Katika kutekeleza majukumu yake, Wakala una matarajio yafuatayo:

1.      Kusimamia sera na mpango mkakati wa miaka mitano (5) ili kuhakikisha kuwa utekelezaji wake unafikia malengo yaliyo kusudiwa.

2.      Kuendelea kusimamia viwango vya usalama na afya mahali pa kazi ili kulinda afya za wafanyakazi na kuhakikisha kuwa viwango hivyo vinafuatwa kwa kuandaa sera na miongozo ya usimamizi katika sekta mbali mbali.

3.      Kuendelea kuongeza elimu na ufahamu wa masuala ya afya na usalama mahali pa kazi miongoni mwa waajiri, wafanyakazi na umma kwa ujumla.

4.      Kuendelea kujenga uwezo binafsi wa watumishi wa wakala ili waweze kutoa huduma za afya na usalama na huduma nyingine za wakala kwa ufanisi wa hali ya juu.

Mwaliko

Mwaka huu Wakala unafanya maadhimisho ya miaka kumi na tano tangu kuanzishwa kwake katika kanda zake zote sita. Hapa Dodoma watumishi wa Wakala wanatarajia kushirikiana kufanya usafi wa standi ya Mabasi ya mkoa na maeneo yanayozunguka hiyo standi. Tukionyesha namana sahihi ya kufanya usafi kwa kuzingatia misingi ya afya na usalama kazini na tutawaeleimisha wafanyausafi masuala ya kuzingatia wanapofanya usafi huo. Aidha katika ofisi zetu mikoani zoezi kama hili litafanyika pia kwa kushirikiana na wadau waliopo katika kanda hizo, mfano kwa kanda ya Pwani watumishi wa wakala waliopo mkoani Dar es salaam watashiriki kufanya usafi hospitali ya Mwananyamala na kutoa msaada wa vifaa kinga hapo hospitalini. Wote Mnakaribishwa sana.

Baada ya kusema hayo asenteni kwa kunisikiliza


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu

Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu

MHE. Jenista Mhagama (Mb)


Una Malalamiko?
Unataka kutoa taarifa ya Tukio au Ajali eneo la kazi?