• +255-22-2760548/2760552
  • info@osha.go.tz

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

COVID-19

 

Emergency

TAARIFA KWA UMMA

UTEKELEZAJI WA MAELEKEZO YA SERIKALI KATIKA KUDHIBITI VIRUSI VYA CORONA VINAVYOSABABISHA  HOMA KALI YA MAPAFU (COVID-19)

DAR ES SALAAM APRIL 21, 2020:

Kufuatia maagizo ya serikali kuhusu hatua za kujikinga na kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa homa kali ya mapafu (CPVID-19) unaosababishwa na Virusi vya corona, Menejimenti ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA), inapenda kuwajulisha wadau wake na wananchi kwa ujumla mambo yafuatayo.

  1. Kuanzia Tarehe 22 April 2020Wageni wanaofika katika Ofisi za OSHA kote nchini watatakiwa kuvaa barakoa pamoja na kufuata maelekezo mengine yatayotolewa na wahudumu wetu ikiwemo kutakiwa kupimwa kiwango cha joto la Mwili.
  2. Ii Kupunguza Msongamano katika Ofisi zetu, tunahimiza wadau wetu kutumia njia mbadala za mawasiliano kupata huduma zetu zikiwemo kupiga simu Bila Malipo (0800110091 au 0800110092 ) , kutumia Barua pepe (info@osha.go.tz) au   au kutembelea tovuti yetu (www.osha.go.tz) na mitandao yetu ya kijamii kwaajili ya kupata taarifa mbalimbali pamoja na fomu za usajili wa maeneo ya kazi.
  3. OSHA itaendelea kufanya kaguzi katika maeneo yote ya kazi, kuangalia utekelezaji wa wa Sheria ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi pamoja na maelekezo ya serikali katika kudhibiti virusi vya corona kuenea mahali pa kazi.

Aidha, tunakumbusha wamiliki ama wasimamizi wa maeneo yote ya Kazi kuzingatia maelekezo ya kujikinga, Kuwakinga wafanyakazi na watu wengine wanaotembelea katika maeneo husika kama yanavyotolewa na viongozi wa juu wa Serikali pamoja na Wizara ya Afya ikiwemo kuosha mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni, Kutumia vitakasa mikono (Hand Sanitizer) na kuepuka mikusanyiko isyo ya Lazima.   

 

Usalama na Afya Kazini Unaweza Kuokoa Maisha , Tanzania bila Corona Inawezekana

sote Tujikinge na Kuchukua Tahadhari 

Imetolewa na 

KAIMU MTENDAJI MKUU

K.H MWENDA