• +255-22-2760548/2760552
 • info@osha.go.tz

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

MAFUNZO YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI


RATIBA YA MAFUNZO YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI BOFYA KUPAKUA


FOMU YA MAOMBI YA MAFUNZO YA USALAMA NA AFYA BOFYA KUPAKUA


 

MAFUNZO

Kwanini mafunzo kuhusu usalama na afya ni muhimu?                                                                                                                   

Mafunzo sahihi kuhusu usalama na afya ya wafanyakazi husaidia kuongeza motisha ambayo hupelekea kukua kwa tija. Tija ikiongezeka faida nayo huongezeka. Kwa upande mwingine, athari na magonjwa vikipungua kampuni hulipa viwango vidogo zaidi vya bima ya afya.  Yote haya yakitokea pande zote zinafaidika.

Utoaji wa mafunzo ya usalama na afya ni miongoni mwa majukumu muhimu ya OSHA ambayo huunda sehemu ya mamlaka yake. OSHA inatoa mafunzo kuhusu usalama na afya kwa wafanyakazi na watu wenye jukumu la kusimamia afya na usalama mahala pa kazi. OSHA inachukulia mafunzo kuhusu usalama na afya kama sehemu mojawapo ya programu za usalama na afya za OSHA zilizoandaliwa kwa ajili ya kuhakikisha usalamana afya ya wafanyakazi. Kwa maana hii, OSHA inahimiza waajiri kutoa mafunzo mahsusi kwa wafanyakazi ambao kazi zao ni hatarishi kabla ya hawajaanza kufanya kazi zenye athari hasi na hutoa huduma za ugani na elimu kwa umma kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu usalama na afya mahala pa kazi. Lengo kuuni kuwalinda wafanyakazi dhidi ya athari hasi, magonjwa na vifo vinavyotokana na kazi wanapokuwa kazini.

Mafunzo yanayotolewa mahala pa kazi (In-house/On site) 

Kozi ambazo ni mahsusi kwa ajili ya wafanyakazi zinaweza kutolewa mahala pa kazi. Faida kuu ya aina hii ya mafunzo ni kwamba mafunzo yanaundwa kukidhi mahitaji ya mteja (mwajiri) na yanaweza kutolewa kwa kutumia mifano halisi ya sera na taratibu za kazi za eneo la kazi husika.

Mafunzo yanayotolewa mahala pa kazi linasaidia pia kupunguza ghrama kwani yanaweza kutolewa kwa watu wengi kwa wakati mmoja ukilinganisha na mafunzo ambayo mfanyakazi mmoja au kikundi kidogo cha wafanyakazi wanahudhuria nje ya mahala pa kazi. Hata hivyo, masharti ya kutoa mafunzo kama haya ni kwamba ni lazima  pawepo na washiriki angalau 30, chumba kinachofaa kwa ajili ya mafunzo na viburudisho kwa ajili ya washiriki.

Mafunzo yanayotolewa nje ya mahala pa kazi

Tunatoa mafunzo ya aina gani kuhusu usalama na afya mahala pa kazi?

Programu zetu zote za mafunzo zinaratibiwa na Mkurugenzi wa Mafunzo, Utafiti na Takwimu na zinajumuisha mafunzo yaliyopangwa na mafunzo mahsusi kulingana na mahitaji ya waajiri kama ilivyooneshwa hapa chini:-

SN COURSE FEES DURATION
1. National Occupational Safety and Health Course –NOSHC-I  690,000 15 days (3 weeks)
2. National Occupational Safety and Health Course –NOSHC-II 690,000 15 days (3 Weeks)
3. OHS Risk Assessment 500,000 Siku 5
4. Working at Height 300,000 Siku 4
5. Safety and Health Representative  250,000 Siku 4
6. Safe use of Chemicals at Work 250,000 Siku 4
7. OHS in Construction Industry 250,000 Siku 4
8. Accident Investigation 400,000 Siku 3
9. Industrial First Aid 250,000 Siku 3
10. Safety in Lifting Appliance 250,000 Siku 4
11. Safe Boiler Operation 300,000 Siku 4
12. General OHS awareness  120,000 Siku 1

Kumbuka: Kozi zote zinaweza kuendeshwa mahali popote nchini Tanzania isipokuwa kozi ya NOSHC I na II ambazo zinatolewa tu katika ofisi za Makao Makuu ya OSHA zilizopo Kinondoni, Dar es Salaam. 

JINSI YA KUOMBA NA KUSHIRIKI MAFUNZO

Kalenda ya mafunzo na fomu ya maombi vinapatikana katika ofisi za OSHA Makao Mkuu zilizopo Kinondoni Manyanya jijini Dar es Salaam au kutoka katika ofisi za OSHA za kanda jijini Arusha, Mwanza, Mtwara, Mbeya na Dodoma. Kalenda ya Mafunzo na Fomu ya Maombi vinaweza pia kupakuliwa kutoka katika tovuti ya OSHA www.osha.go.tz [insert link to Forms] 

Walengwa wa kozi zetu ni nani? 

 • Mfanyakazi yeyote kutoka sekta yoyote 
 • Watu wenye majukumu ya kusimamia masuala ya usalama na afya mahala pa kazi 
 •  Wajasiriamali wadogo na wakubwa  
 •  Mtu mwenye nia ya kufanya kazi kama Afisa/Meneja Usalama na Afya 
 •  Wakurugenzi Wakuu na Menejimenti kutoka mashirika ya umma na binafsi 

Faida ya Mafunzo ya Afya na Usalama 

 • Yanawapa wafanyakazi maarifa ya kusimamia afya na usalama kwa ufanisi. 
 • Yanawasaidia wafanyakazi wafanye kazi kwa usalama na kuwa huru kutokana na hatari ya kupata athari hasi/majeraha na magonjwa. 
 • Yanajenga utamaduni wa usalama na afya katika maisha ya kila siku. 
 • Yanatoa masharti ya kisheria kuhusu usalama na afya ya wafanyakazi. 
 • Yanasaidia kuzuia au kupunguza gharama zinazotokana na ajali na mgaonjwa mahala pa kazi. 
 • Yanaongeza tija na motisha ya wafanyakazi.