• +255-22-2760548/2760552
  • info@osha.go.tz

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

Mkataba Huduma kwa Mteja

DIBAJI

Mkataba huu wa Huduma kwa Mteja wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umeandaliwa kama sehemu ya jitihada zake endelevu katika kutoa huduma bora ili kukidhi mahitaji ya wateja wake. Mkataba huo unatoa mwongozo baina ya watumishi wa OSHA na wateja kuhusu huduma za Usalama na Afya kazini.

Mchakato wa kuandaa mkataba huu ulizingatia viwango vya ndani na vya kimataifa vinavyohusu kada ya Usalama na Afya mahali pa kazi. Baadhi ya vigezo vilivyozingatiwa katika kuandaa, kupitia na kuboresha maudhui ya mkataba huu ni pamoja na kupata maoni kutoka kwa uongozi wa juu wa Wakala, watumishi wengine pamoja na wadau mbali mbali.

Hatua hizi zilizingatiwa ili kuhakikisha kwamba maudhui ya mkataba huu yanakuwa ya kina, yenye mawazo bora na kusimamiwa ipasavyo. Jambo ambalo litasaidia katika kuongeza ufanisi wa Wakala katika utoaji wa huduma na kufanya maboresho muhimu kwa kadri ya mahitaji ya wateja wetu.