• +255-22-2760548/2760552
 • info@osha.go.tz

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

Mwongozo wa Wafanyakazi

Tafsiri:

Mtu yeyote anaajiriwa na mtu mwigine, kampuni au shirika kufanya kazi maalum/mahsusi na kupata ujira kwa kazi hiyo anajulikana kama mfanyakazi. 

Haki na Majukumu:

Haki:

Chini ya sheria ya OSHA, wafanyakazi wanayo haki ya kufanya kazi katika mazingira ambayo hakuna uwezekano wa kupata madhara/athari hasi.

Hususan, wanayo haki ya kufanya mambo yafuatayo:

 1. Kupeleka maombi ya siri OSHA kuomba ukaguzi wa sehemu yao ya kazi.
 2. Kupokea taarifa na mafunzo kuhusu athari, mbinu za kuzuia madhara, na viwango vya OSHA vinavyohusu sehemu zao za kazi. Hata hivyo, mafunzo yanapaswa kutolewa kwa lugha na misamiati ambayo wafanyakazi wanaweza kuelewa.
 3. Kupeleka malalamiko OSHA endapo mwajiri wao amekosa kuwatendea haki kwa kuwa wametumia haki zao zozote chini ya Sheria ya OSHA.
 4. Kupeleka malalamiko OSHA endapo mwajiri wao amelipiza kisasi kwa kuwafukuza kazi,kuwashusha cheo, kuwahamisha au kutowatendea haki kwa namna yoyote ile kwasababu walitoa taarifa ya siri kuhusu ukiukwaji wa masharti ya usalama na afya mahala pa kazi. 

Majukumu:

Sheria ya OSHA ya mwaka 2003, inaeleza kazi na majukumu ya wafanyakazi katika Kipengele cha93 na 99. Chini ya sheria hii, wafanyakazi wanayo haki ya kufanya kazi katika mazingira ambayo hayasababishi madhara makubwa.

Maeneo mahsusi yanayohusu majukumu ya wafanyakazi ni haya yafuatayo:

 1. Kutumia  kwa usahihi vifaa kinga binafsi na vifaa vingine vinavyohusu ustawi wao kama ilivyoelezwa.
 2. Kuepuka kujiweka wao wenyewe pamoja na wafanyakazi wengine katika hali ya hatari;
 3. Kuepuka kutumia vibaya vifaa vilivyowekwa kwa ajili ya usalama.
 4. Kushirikiana na mwajiri katika masuala yanayohusu usalama.
 5. Kuwa mwangalifu kuhusu afya na usalama binafsi na usalama na afya ya wafanyakazi wengine (wajibu wa kuzingatia kanuni ya uangalifu).
 6. Kutoa taarifa kwa Mkaguzi endapo mwajiri anashindwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Osha ya mwaka 2003 masharti mengine yoyote ya kisheria.
 7. Kutoa taarifa kwa mwajiri au msimamizi endapo wamepatwa na janga au ajali mahala pa kazi.
 8. Kutii maagizo ya kisheria yanayotolewa na kutii sheria za wafanyakazi na taratibu zinazotolewa na mwajiri.

Kwa taarifa zaidi kuhusu haki na wajibu wa mfanyakazi rejea hapa …. [link]