• +255-22-2760548/2760552
 • info@osha.go.tz

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

Muundo wa Wakala

MUUNDO WA WAKALA

Dhima

Kuhakikisha usalama na afya ya wafanyakazi Tanzania Bara kwa kudhibiti, kusimamia utekelezaji, na kuendeleza viwango imara vya Usalama na Afya kazini kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Dira

Kuhakikisha sehemu za kazi ni salama na zenye Afya

Maadili

 • Uwazi
  Tunaendesha shughuli zetu kwa uwazi na kwa namna inayoelekeza na kushirikishana taarifa baina ya idara zote ndani ya taasisi 
 • Ustadi
  Tunatekeleza kazi na majukumu yetu kulingana na taratibu na viwango vilivyowekwa.
 • Uwajibikaji
  Tunawajibika kwa matokeo ya shughuli zetu na tunawaheshimu wadau wote wa ngazi zote za uendeshaji.
 • Uadilifu
  Tunazingatia haki, usawa na uaminifu kwa wateja wetu wote.
 • Kufanya kazi pamoja kama timu
  Tunaheshimu na kutambua nguvu na uwezo tofauti wa kila mfanyakazi.

 

Mambo tunayofanya

 • Usajili wa mahala pa kazi 
 • Ukaguzi wa kisheria wa mahala pa kazi (Ukaguzi wa Jumla, Ukaguzi wa Mitambo, Ukaguzi wa Usalama wa Umeme, Tafiti zinazohusu Usafi Viwandani, Uchunguzi wa Mwili, Ukaguzi wa Majengo na Ujenzi na  Ukaguzi wa mazingira kwa maana ya hali na ufanisi wa vifaa/mashine zinavyohusiana na mwili wa binadamu, k.v. kompyuta, dawati, kiti, meza, n.k.)
 • Mafunzo ya kukuza ufahamu kuhusu afya na usalama 
 • Uchunguzi wa michoro ya mahala pa kazi ili kuhakikisha mahitaji ya kiafya na kiusalama yanazingatiwa 
 • Uchunguzi wa ajali zinazotokea mahala pa kazi 
 • Kutoa ushauri husika na masuala ya sheria na kanuni
 • Kuandaa miongozo kutokana na Mahitaji ya sheria na kanuni