• +255-22-2760548/2760552
  • info@osha.go.tz

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

Ofisi za Kanda

Wasifu wa Ofisi za Kanda 

 

Kama njia mojawapo ya kusambaza huduma zake nchini kote, OSHA Iliona umuhumu wa kuandaa mpango wa uendeshaji ambao ni rahisi na wenye ufanisi kwa ajili ya kuendesha shughuli zake na iliamua kuunda mtandano wa ofisi za kanda unaounganisha OSHA na wateja wake. 

Mkoa wa Dar es Salaam ulionekana kuwa mahali mwafaka kwa ajili ya makao makuu ya taasisi; ikisaidiwa na ofisi sita za kanda zinazohudumia maeneo ya kanda ya Pwani, kanda ya Kati,  kanda ya Kaskazini, kanda ya Ziwa, kanda ya Kusini na kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

 

KANDA YA PWANI

Kanda hii inaundwa na mikoa mitatu, yaani mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro. Ofisi za makao makuu ya kanda hii zipo katika Jiji la kibiashara la Dar es Salaam na ofisi ndogo iko katika mkoa wa Morogoro. Shughuli kuu za uchumi katika kanda hii ziko katika sekta ya viwanda na biashara. Kwa maana hiyo, shughuli za OSHA katika kanda hii zinalenga kuboresha usalama na afya ya wananchi wanaojishughulisha na shughuli za uzalishaji wa viwandani pamoja na biashara mbalimbali. Sifa kuu ya kanda hii ni kwamba inasimamia zaidi ya asilimia 80 ya sehemu za kazi zilizosajiliwa na OSHA. Ili kuwasiliana na ofisi za kanda hii bonyeza hapa.

 

KANDA YA KASKAZINI 

Kanda ya Kaskazini inaundwa na mikoa minne, ambayo ni; Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga. Ofisi za makao makuu ya kanda hii zipo Arusha kwenye makutano ya barabara ya Uhuru/Metropol na ofisi ndogo iko katika mkoa wa Tanga. Sifa kuu ya kanda hii ni uwepo wa shughuli nyingi zinazohusiana na biashara ya utalii, kwani kuna vivutio vingi vya watalii kama vile Mbuga za Wanyama za Tarangire, Ngorogoro na Serengeti, tukitaja baadhi tu. OSHA ina jukumu kubwa katika kuhakikisha usalama na afya ya wafanyakazi na wananchi wengine wanaojishughulisha na sekta ya utalii na shughuli  nyingine za kiuchumi katika kanda hii. Ili kuwasiliana na ofisi za kanda hii bonyeza hapa.

 

KANDA YA ZIWA

Kanda hii imeundwa na mikoa ya Mwanza, Geita, Shinyanga, Simiyu, Kagera na Mara. Ofisi za makao makuu ya kanda zipo katika Jiji la Mwanza barabara ya Stesheni na ofisi ndogo iko mjini Bukoba mkoani Kagera. Kanda hii inajulikana kwa shughuli za kiuchumi zinazohusiana na madini na inazo kampuni kubwa zinazojishughulisha na uchimbaji wa madini zinazofanya shughuli zake katika mikoa mbalimbali ndani ya kanda hii. OSHA inahusika na usalama na afya za wafanyakazi wa makampuni ya uchimbaji wa madini pamoja na wachimbaji wadogo na wa kati. Hivyo, inahakikisha kwamba watu wanaofanya kazi katika migodi na sekta nyingine wanafuata sheria na kanuni za usalama na afya. 

 

KANDA YA KATI

Kanda hii inaundwa na mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora na Kigoma na ofisi kuu ya kanda ipo Jijini Dodoma barabara ya Askari. Makao Makuu ya nchi Tanzania yako katika kanda hii na ndipo ofisi kuu za makao makuu ya kanda zilipo. Zipo shughuli za kiuchumi mchanganyiko kuanzia shughuli za kilimo, yakiwemo mashamba mashuhuri ya zabibu hadi shughuli za kibiashara ambazo zinafaidika kutokana na kwamba mkoa wa Dodoma upo katikati ya mikoa mingine. OSHA inahakikisha usalama na afya ya wafanyakazi wanaofanya shughuli mbalimbali za kiuchumi katika kanda hii. 

 

KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI

Hii ni miongoni mwa kanda kubwa nchini ambayo inaundwa na mikoa sita, yaani; Mbeya, Iringa, Katavi, Njombe, Songwe na Rukwa. Ofisi za makao makuu ya kanda zipo katika Jiji la Mbeya mtaa wa Uzunguni. Shughuli kuu ya kiuchumi katika kanda hii ni kilimo kutokana na uwepo wa udongo mzuri wenye rutuba. Vyakula vingi vikuu vinalimwa katika kanda hii. Zipo pia shughuli mbalimbali za kiuchumi kama vile biashara, uzalishaji, misitu na madini. OSHA inajitahidi kuinua uelewa kuhusu umuhimu wa usalama na afya miongoni mwa wadau mbalimbali katika kanda hii, inafanya ukaguzi na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu namna ya kuboresha usalama na afya mahali pa kai miongoni mwa watu waishio katika mikoa ya nyanda za juu kusini.

 

KANDA YA KUSINI

Kanda hii inaundwa na mikoa mitatu ya Mtwara, Lindi na Ruvuma. Makao makuu ya kanda hii yapo Mtwara. Wengi wa wakazi wa kanda hii ni wakulima wa korosho lakini kanda hii inajulikana pia kwa kuwa na viwango vikubwa vya gesi asilia. Shughuli zote hizi za kiuchumi zinahitaji mifumo thabiti ya kuhakikisha ufuataji wa sheria, kanuni na viwango vya usalama na afya ya watu wanaojishughulisha na shughuli hizo muhimu za kiuchumi. Shughuli nyingine zinazoendeshwa katika kanda hii ni pamoja na biashara na uzalishaji wa viwandani.

 

ANUANI ZA OFISI 

Kanda ya Pwani – inajumuisha mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro Kanda ya Kaskazini – inajumuisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga
Mahali Makao makuu ya OSHA yapo Kitalu Na. MNY/KMB/565, Barabara ya Mahakama – Kinondoni Mahali Arusha – Br. Uhuru /Eneo la Metropol
Anwani ya posta S.L.P 519, Dar es Salaam Anwani ya posta S.L.P 47, Arusha
Simu +255 (0) 22 2760548 Simu +255 (0) 27 2546255
Nukushi +255 (0) 22 2760552 Nukushi +255 (0) 27 2546255
Barua pepe info@osha.go.tz Barua pepe info@osha.go.tz
Kanda ya Ziwa – inajumuisha mikoa ya Mwanza, Geita, Shinyanga, Simiyu, Kagera na Mara Kanda ya Kati – inajumuisha mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora na Kigoma
Mahali Mwanza Br. Stesheni Mahali Dodoma Barabara ya Mahakama. Kitalu. 556 eneo la kilimani.
Anwani ya posta S.L.P 3087, Mwanza Anwani ya posta S.L.P 1818, Dodoma
Simu +255 (0) 28 2500368 Simu +255 (0) 26 2320205
Nukushi +255 (0) 28 2500368 Nukushi +255 (0) 26 2320205
Barua pepe info@osha.go.tz Barua pepe info@osha.go.tz
Kanda ya Nyanda za Juu Kusini – inajumuisha mikoa ya Mbeya, Iringa, Katavi, Njombe, Songwe na Rukwa  Kanda ya Kusini – inajumuisha mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma 
Mahali Mbeya – Mtaa wa Uzunguni Mahali Mtwara – Br. Makonde
Anwani ya posta S.L.P 880, Mbeya Anwani ya posta S.L.P 793, Mtwara
Simu +255 (0) 25 2502626 Simu +255 (0) 23 2334696
Nukushi +255 (0) 25 2502626 Nukushi +255 (0) 23 2334696
Barua pepe info@osha.go.tz Barua pepe info@osha.go.tz