Hii ni miongoni mwa kanda kubwa nchini ambayo inaundwa na mikoa sita, yaani; Mbeya, Iringa, Katavi, Njombe, Songwe na Rukwa. Ofisi za makao makuu ya kanda zipo katika Jiji la Mbeya mtaa wa Uzunguni. Shughuli kuu ya kiuchumi katika kanda hii ni kilimo kutokana na uwepo wa udongo mzuri wenye rutuba. Vyakula vingi vikuu vinalimwa katika kanda hii. Zipo pia shughuli mbalimbali za kiuchumi kama vile biashara, uzalishaji, misitu na madini. OSHA inajitahidi kuinua uelewa kuhusu umuhimu wa usalama na afya miongoni mwa wadau mbalimbali katika kanda hii, inafanya ukaguzi na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu namna ya kuboresha usalama na afya mahali pa kai miongoni mwa watu waishio katika mikoa ya nyanda za juu kusini.