• +255-22-2760548/2760552
  • info@osha.go.tz

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

Siku ya Kilele 2020

Tuzo Mwaka 2020

Maonesho 26 Aprili 2020

Ukaguzi wa Usalama na Afya

Mkurugenzi wa Usalama na Afya wa OSHA, Alexander Ngata, akifanya majadiliano na maofisa wa kiwanda kabla ya kuanza kufanya ukaguzi katika kiwanda.

 

 

Mafunzo ya Huduma ya Kwanza

Mkufunzi wa Huduma ya Kwanza wa OSHA, Kassim Mtema, akionyesha kwa vitendo namna ya kumhudumia majeruhi wa ajali katika sehemu ya kazi.

Kutoa Elimu ya Usalama na Afya kwa Umma

Mkaguzi wa Mazingira wa OSHA, Simon Lwaho, akimkabidhi mteja kabrasha lenye machapisho ya OSHA baada ya mteja huyo kutembelea banda la OSHA na kujipatia elimu wakati wa maonesho ya Nane Nane jijijni Mbeya.

Usalama Viwandani

Wafanyakazi waliokingwa ipasavyo wakitekeleza majukumu yao kiwandani. Wafanyakazi wanaokingwa ipasavyo dhidi ya vihatarishi vya kiusalama na afya hufanya kazi kwa bidii na kujiamini na hivyo kuongeza tija katika uzalishaji.<...

Ujumbe wa Mtendaji Mkuu

Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) ni chombo cha kusimamia usalama na afya mahala pa kazi kwa kuhakikisha kwamba waajiri wote nchini wanaweka miundo na mifumo inayohakikisha usalama na afya mahala pa kazi vinalindwa.  

Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la idadi ya waajiri wanaotuma maombi kuomba kukaguliwa au mafunzo ya usalama na afya makazini mwao. Hiki ni kiashiria muhimu cha mafanikio. Taasisi ya OSHA inatia mkazo katika kuelimisha kuliko kuadhibu ili kuhakikisha kwamba waajiri wanawajibika bila shurti.  

Hata hivyo, bado tunakabiliwa na changamoto kuu mbili; i) uelewa mdogo miongoni mwa waajiri na wafanyakazi kuhusu umuhimu wa kuzingatia masuala ya usalama na afya kazini, na ii) ukiukwaji wa masharti kwa kutozingatia viwango vya usalama na afya. Changamoto ya pili inatokana na imani isiyo sahihi miongoni mwa baadhi ya waajiri kwamba gharama za kuhakikisha usalama na afya mahala pa kazi ni kubwa sana, tofauti na hali halisi inavyoonesha. Utafiti umethibitisha kwamba faida zitokanazo na mazingira ya usalama na afya mahala pa kazi ni kubwa kuliko gharama. 

Maelezo Zaidi

Takwimu za Mwaka wa Fedha 2018/2019

0000

Maeneo yaliyosajiliwa

0000

Ajali zilizoripotiwa

0000

Kaguzi Zilizofanyika

0000

Maeneo yaliyokidhi Viwango

Habari Mpya

Wajasiriamali wadogo zaidi ya 450 wanufaika na mafunzo ya OSHA

Zaidi ya wajasiriamali wadogo 450 wamenufaika na mafunzo ya Usalama na Afya kazini ambayo yametolewa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi...
Endele kusoma

RC awataka waajiri kutekeleza Sheria ya Afya na Usalama kazini

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, amewaagiza wamiliki wa viwanda kutekeleza ipasavyo Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa kazi yenye lengo l...
Endele kusoma