Mafunzo sahihi kuhusu usalama na afya ya wafanyakazi husaidia kuongeza motisha ambayo hupelekea kukua kwa tija. Tija ikiongezeka faida nayo huongezeka. Kwa upande mwingine, athari na magonjwa vikipungua kampuni hulipa viwango vidogo zaidi vya bima ya afya. Yote haya yakitokea pande zote zinafaidika.
Utoaji wa mafunzo ya usalama na afya ni miongoni mwa majukumu muhimu ya OSHA ambayo huunda sehemu ya mamlaka yake. OSHA inatoa mafunzo kuhusu usalama na afya kwa wafanyakazi na watu wenye jukumu la kusimamia afya na usalama mahala pa kazi. OSHA inachukulia mafunzo kuhusu usalama na afya kama sehemu mojawapo ya programu za usalama na afya za OSHA zilizoandaliwa kwa ajili ya kuhakikisha usalamana afya ya wafanyakazi. Kwa maana hii, OSHA inahimiza waajiri kutoa mafunzo mahsusi kwa wafanyakazi ambao kazi zao ni hatarishi kabla ya hawajaanza kufanya kazi zenye athari hasi na hutoa huduma za ugani na elimu kwa umma kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu usalama na afya mahala pa kazi. Lengo kuuni kuwalinda wafanyakazi dhidi ya athari hasi, magonjwa na vifo vinavyotokana na kazi wanapokuwa kazini.
OSH Training programmes provided by OSHA
Working at Height October 04, 2024 - October 08, 2024 - Arusha-Hazina Ndogo-Arusha