Occupational Safety and Health Authority
  +255-22-2760548 / 2760552       info@osha.go.tz                     

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

Draft OHS Regulation

MWALIKO KWA WADAU KUWASILISHA MAONI YAO KUHUSU RASIMU ZA KANUNI SITA (6) ZA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

OSHA ni Taasisi ya serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) ambayo jukumu lake la msingi ni kusimamia utekelezaji wa Sheria Na. 5 ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003 pamoja na kanuni zake. Lengo la sheria hii ni kuhakikisha kwamba wafanyakazi wanalindwa dhidi ya vihatarishi vilivyopo katika sehemu za kazi ambavyo vinaweza kusabisha magonjwa, ajali au vifo.

Kanuni mbalimbali ambazo hutekelezwa sambamba na Sheria tajwa huandaliwa na Wizara inayohusika na Masuala ya Kazi nchini pamoja na wataalam toka OSHA ambao huandaa rasimu za kanuni hizo na kuzipeleka kwa wadau kwa ajili ya kupata maoni yao kabla ya kuidhinishwa na Baraza la Masuala ya Kazi, Uchumi na Jamii (LESCO) lililopo chini ya Wizara husika.

Kwasasa OSHA ina jumla ya kanuni 9 zikiwemo kanuni ya Usalama na Afya katika sekta ya ujenzi, Usimamizi wa Jumla wa sehemu za kazi, kanuni ya uwasilishaji taarifa za ajali, magonjwa na matukio hatarishi pamoja na kanuni ya usalama na afya katika vifaa vya kunyanyulia mizigo mizito. Aidha, uandaaji wa rasimu za kanuni zaidi unaendelea kufanyika kwa kadri ya mahitaji ambapo Wizara pamoja na wataalam kutoka OSHA imeandaa rasimu sita (6) za kanuni mpya ambazo zinahitaji maoni ya wadau kwa ajili hatua zaidi. Kanuni hizo ni pamoja na; kanuni ya huduma za afya mahali pa kazi, usalama na afya katika ufanyaji kazi kwenye majukwaa, matumizi ya kemikali hatarishi, maafisa usalama mahali pa kazi, kamati za Usalama na Afya mahali pa kazi na Usalama wa umeme na mitambo inayotumia umeme.

Hivyo, Wizara Wizara inapenda kuwaalika wadau wote kupakua rasimu za kanuni tajwa katika tovuti (www.osha.go.tz), kuzipitia na kisha kutuandikia maoni yao na kuyawasilisha kwa njia ya mtandao kupitia barua pepe ifuatayo; (info@osha.go.tz). Zoezi hili la kupokea maoni litafanyika kuanzia Septemba 21, 2021 hadi Novemba 22, 2021.

Ndugu mdau, maoni yako ni muhimu sana katika kukamilisha uandaaji wa kanuni hizi kwa minajili ya kuboresha mazingira ya kazi na hivyo kuimarisha hali ya usalama na afya katika sehemu zote za kazi hapa nchini.

Nyote mnakaribishwa

Kwa ufafanuzi au msaada zaidi, tafadhali wasiliana nasi: 0735000449 na 0715017474

Send Your Comments About Regulation Change

mLQ2LWu6IJVlNzEMPgOl1BtQhlgFKJmPJGsx2cYt