Occupational Safety and Health Authority
  +255-22-2760548 / 2760552       info@osha.go.tz                     

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

Our Services


Huduma Zetu

services

Kusajili sehemu za kazi

Kwa mujibu wa kifungu Na. 16 cha Sheria Na. 5 ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003, wamiliki au wasimamizi wa sehemu zote za kazi nchini wanapaswa kuhakikisha kwamba maeneo husika ya kazi yanasajiliwa na OSHA ili kuiwezesha Taasisi kuwafikia kwa ajili ya kuwapa huduma nyinginezo za masuala ya Usalama na Afya mahali pa kazi.

services

Ukaguzi wa Usalama na Afya mahali pa kazi

OSHA hufanya ukaguzi mbalimbali katika sehemu za kazi ili kuhakikisha kwamba kunakuwa na mifumo madhubuti ya Usalama na Afya mahali pa kazi kwa ajili ya kulinda nguvukazi dhidi ya ajali, magonjwa, vifo vinavyoweza kusababishwa na mazingira ya kazi yasiyo rafiki.

services

Kukuza uelewa wa masuala ya Usalama na Afya miongoni mwa wadau

Miongoni mwa majukumu ya OSHA ni kukuza uelewa wa masuala ya Usalama na Afya mahali pa kazi kupitia mafunzo, maonesho, makongamano, majarida, vipeperushi, vipindi vya luninga na redio lengo likiwa ni kujenga uelewa wa pamoja katika masuala husika na hivyo kila mtu kuweza kushiriki kikamilifu katika kujenga nguvu kazi salama na yenye afya njema kwa maendeleo endelevu ya Taifa letu. 

services

Uchunguzi wa afya za wafanya

Uchunguzi wa afya za wafanyakazi ambao hutekelezwa na wakaguzi wa afya wa OSHA hufanyika katika hatua tatu (3) muhimu ambazo ni; kabla ya kuanza kazi, mfanyakazi akiwa kazini na mfanyakazi anapoachana na mwajiri wake kwa sababu mbalimbali ikiwemo kustaafu, kuacha kazi, kuondolewa kazini. Jambo hili hufanyika ili kutambua endapo afya ya mfanyakazi inamuwezesha kumuda majukumu anayokabidhiwa na mwajiri wake pamoja na kutambua endapo mfanyakazi amepata athari zozote kutokana na mazingira ya kazi yasiyo rafiki.

VIGEZO VYA KUPATA CHETI CHA ITHIBATI (OHS COMPLIANCE)

compliance

Sajili eneo lako la kazi na kupatiwa cheti cha usajili

compliance

Fanya tathmini ya hatari za usalama na afya katika eneo lako la kazi walau mara moja kwa mwaka

compliance

Andaa sera ya Usalama na Afya katika eneo la kazi husika

compliance

Hakikisha kwamba eneo lako la kazi limefanyiwa ukaguzi wa usalama na afya na wakaguzi stahiki kwa mujibu wa Sheria ya Afya na Usalama ya mwaka 2003

compliance

Hakikisha kwamba wafanyakazi wako wamefanyiwa uchunguzi wa afya zao kulingana na majukumu yao

compliance

Hakikisha wawakilishi wa usalama na afya eneo la kazi pamoja na watoa huduma ya kwanza uliowateua wamehudhuria na kupata vyeti vya mafunzo stahiki yanayoratibiwa na OSHA