Occupational Safety and Health Authority
  +255-22-2760548 / 2760552       info@osha.go.tz                     

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

image

WAJASIRIAMALI 250 WANUFAIKA NA MAFUNZO YA USALAMA NA AFYA ARUSHA

Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi OSHA imeendelea na kampeni ya uhamasishaji wa uwepo wa mazingira salama katika maeneo ya kazi ambapo takribani wajasiriamali 250 wamepatiwa mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi Mkoani Arusha.

Kupitia mafunzo hayo yaliyotolewa kwa wajasiriamali hao katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Arusha pamoja na AICC Club yalilenga kuwajengea wajasiriamali hao uelewa juu ya masuala mbalimbali ikiwemo Sheria na Miongozo mbalimbali ya usalama na afya mahali pa kazi, utambuzi wa vihatarishi mbalimbali vinavyowakabili na njia sahihi za kuvidhibiti vihatarishi hivyo pamoja na Mafunzo ya huduma ya kwanza kwa watu waliopatwa na changamoto mbalimbali za kiafya katika maeneo ya kazi.

“Mafunzo haya yatawasaidia wajasiriamali hawa kutekeleza majukumu yao wakiwa salama dhidi ya vihatarishi mbalimbali vya ajali na magonjwa vilevile wataweza kuzalisha kwa tija hivyo kuongeza ushindani wa bidhaa zao wanazo zizalisha katika masoko mbalimbali” Alisema Emakulata Longido muwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka OSHA.

kwa upande wake Moteswa Meeda ambeye aliwasilisha mada juu ya ya huduma ya kwanza wa watu waliopatwa na changamoto mbalimali za kiafya amesema kuwa kupitia mada aliyowasilisha imewajengea uelewa juu ya masuala mbalimbali ikwemo huduma ya kwanza kwa mtu aliyedhurika na kemikali au kunywa sumu, aliyeungua na moto n.k

Aidha, Husna Abubakari ni kiongozi wa umoja wa wajasiriamali wa Mkoa wa Arusha amekiri kuwa mafunzo hayo yatakuwa na msaada mkubwa sana kwa wajasiriamali hao na yataongeza tija katika uzalishaji wa bidhaa zao kwa kuhakikisha wanafuata miongozo ya masuala ya usalama na afya katika hatua zote kuanzia bidhaa inapoanza kuengenezwa hadi inapomfikia mlaji wa mwisho.