GAWIO KWA SERIKALI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Gawio la Serikali iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Juni, 2025. OSHA chini ya Mtendaji Mkuu, Bi. Khadija Mwenda, ni miongoni mwa Taasisi zilizotoa gawio kwa serikali kiasi cha bilioni 10.4 katika hafla maalum iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam Juni 10, 2025.