MAFUNZO WACHIMBAJI WADOGO BUKOMBE
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Deus Sangu, akikabidhi vifaa kinga na masunduku ya huduma ya kwanza kwa wanachama wa Umoja wa Wanawake Wachimbaji Bukombe (WAWABU)katika hafla ya kufunga mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi yaliyotolewa kwao na OSHA. Vifaa hivyo vilitolewa na OSHA kama sehemu ya programu yao ya mafunzo na kuhamasisha masuala ya usalama na afya miongoni mwa makundi mbalimbali ya wajasiriamali wadogo nchini.