Occupational Safety and Health Authority
  +255-22-2760548 / 2760552       info@osha.go.tz                     

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

OCCUPATIONAL SAFETY AND HEALTH AUTHORITY

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

OCCUPATIONAL SAFETY AND HEALTH AUTHORITY

image

WAWEKEZAJI WAASWA KUTII SHERIA ZA KAZINa Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi - Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Joyce Ndalichako amewataka wawekezaji wa maeneo ya kazi nchini kutekeleza sheria na miongozo mbalimbali ya masuala ya kazi ikiwemo Sheria Na.5 ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya Mwaka 2003.

Ndalichako ametoa agizo hilo mara baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika kampuni za usafirishaji za FAA Logistics, RAPHAEL Logistics pamoja kiwanda cha kutengeneza viroba cha MJM Manufacturing Ltd vya jijini Dar es salaam na kubaini mapungufu makubwa katika usimikaji wa mifumo ya kuwalinda wafanyakazi dhidi ya vihatarishi vya magonjwa na ajali, wafanyakazi kutokuwa na mikataba, waajiri kutowasilisha michango katika mifuko ya hifadhi, pamoja na kutokulipa mishahara kwa wakati na ulimbikizaji wa madeni ya mishahara kwa wafanyakazi wao.

“Tumefanya ziara ya kushitukiza na tumebaini changamoto mbalimbali kwa wafanyakazi wa maeneo haya ya kazi hivyo basi napenda kutoa wito kwa waajiri na wawekezaji wote kuhakikisha wanazingatia sheria na miongozo mbalimbali ya masuala ya kazi lakini pia baada ya ziara hii naziagiza taasisi za OSHA, WCF, NSSF na Idara ya Kazi kurudi mara moja kuendelea na ukaguzi mpaka kufikia ijumaa ya machi 1 ili kushughulikia changamoto hizi kwa kuainisha wafanyakazi wangapi ambao michango yao haiwasilishwi katika mifuko ya hifadhi za jamii na wangapi  hawakatwi kabisa lakini pia kushughulikia usimikaji wa mifumo madhubuti ya masuala ya usalama na afya mahali pa kazi” alisema Prof. Ndalichako, akiongeza kuwa

“Pia ­mfanye ukaguzi ili kutambua malimbikizo ya mishahara na stahiki zingine pamoja na  wafanyakazi wasio na mikataba ili baada ya ripoti ya ukaguzi huu tuweze kutoa amri tekelezi kwa wawekezaji hawa na ndani ya siku thelathini tuweze kufikia makubaliano juu ya utatuzi wa changamoto hizi ”

Aidha ­Profesa Ndalichako amewahasa wafanyakazi katika maeneo yote ya kazi kutoa ushirikiano wa kueleza changamoto zinazowakabili bila uoga huku akiwataka waajiri kuacha mara moja tabia ya kuwaandama wafanyakazi wanao eleza changamoto zao wakati wa ziara za viongozi mbalimbali.

Kwa upade wake Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda amesema kuwa sekta ya usafirishaji ni sekta yenye mchango mkubwa sana katika uchumi wa nchi yetu lakini imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo ziara hiyo ililenga kubaini changamoto hizo na kuona namna gani zinaweza kutatuliwa huku akibainisha kuwa kwa upande wa masuala ya usalama na afya katika kampuni hizo wakaguzi wa OSHA wabebaini kuna mapungufu makubwa katika utekelezaji wa sheria na miongozo ua masuala husika na tayari wametoa hati ya maboresho kwa wawekezaji hao.