Occupational Safety and Health Authority
  +255-22-2760548 / 2760552       info@osha.go.tz                     

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

image

PROF. NDALICHAKO AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA SEKTA BINAFSI KUCHOCHEA AJIRA

Na. Mwandishi wetu – PWANI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amempongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha sekta binafsi ambazo zinachangia kukuza soko la ajira kwa vijana nchini.
Prof. Ndalichako amesema hayo Februari 28,  2024 Wilayani Kibaha alipofanya ziara ya kufuatilia utekelezaji wa sheria za kazi viwandani, akiambana na Maafisa kutoka OSHA, WCF, NSSF na viongozi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Prof. Ndalichako amebainisha kuwa elimu ya ufundi inahitajika viwandani ambapo kupitia Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi inayotolewa kupitia Ofisi hiyo, vijana wanaohitimu wamekuwa wakipata ajira ikiwa ni jitihada za Mhe. Rais ya kuwainua vijana kiuchumi.
Aidha, amewataka wawekazi kuzingatia sheria kazi, kuzingatia masuala ya Usalama na Afya mahali pa Kazi na kutatua changamoto za wafanyakazi ikiwemo kuwapatia mikataba ya kazi, kuwasilisha michango yao NSSF na WCF ili kuwa na uwekezaji wenye tija.
Awali akizungumza Meneja OSHA Kanda ya Pwani Ndg. George Chali amewahimiza wawekezaji kuongeza vifaa kinga kwa wafanyakazi, kuimarisha sehemu za kukaa wafanyakazi ili kuwaepusha na matatizo ya mgongo na kutenga maeneo kwa ajili ya kutoa huduma ya kwanza pindi tatizo linapojitokeza